Mwanaume mmoja ashtakiwa kwa kufichua maelezo mtu mwingine

  • | Citizen TV
    2,915 views

    kesi ambapo mwanamume mmoja ameshtakiwa kwa kufichua maelezo kuhusu mtu mwingine imetajwa hii leo kwenye mahakama ya Milimani kwa mujibu wa mashtaka, Hatim Mohamed Tahir anadaiwa kuwa tarehe 19 mwezi Septemba mwaka wa 2023 akiwa pamoja na mtu mwingine ambaye hakuwa mahakamani, alifichua habari za kibinafsi za roose friedman na mtoto mwingine kwkea wakili Lynn Nganga ambaye alikuwa akisikiza kesi. Hii leo, wakili wake Hatim Tahir, Duncan Okatch alitaka mahakama kuzuia wanahabari kuhudhuria kesi hiyo akisema kuwa mteja wale alikuwa anadhalilishwa. hata hivyo hakimu Ndombi alimtaka mshtakiwa kuwasilisha ombi hilo rasmi. Hatim alipewa dhamana ya shilingi laki tatu. Friedman amemteua wakili Felix Otieno kumwakilisha