Mtoto wake, Hamza Al-Dahdouh, aliuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli akiwa kwenye gari karibu na Rafah pamoja na Mustafa Thuraya, kulingana na maafisa wa afya na umoja wa waandishi wa habari huko Gaza.
Wapalestina wote wawili walikuwa waandishi wa habari wa kujitegemea. Wa tatu alikuwa mwandishi wa kujitegemea ambaye alijeruhiwa.
Al- Dahdouh alikuwa akifanya kazi na Al Jazeera, ambako baba yake Wael Al-Dahdouh ni mwandishi kiongozi wa kituo hicho huko Gaza.
Wael Al-Dahdouh alikuja kuwa mashuhuri kwa watazamaji kote Mashariki ya Kati baada ya kufahamu wakati wa matangazo mubashara kuwa mke wake, mtoto wake mwengine wa kiume, binti yake na mjukuu wake wa kiume walikuwa wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli.
Al-Dahdouh alisema: “Vipi mtu anaweza kupokea habari za kifo cha mtoto wake wa kwanza wa kiume na ndiyo kila kitu katika maisha yangu baada ya kuwapoteza baadhi ya wanafamilia wangu; mke wangu, mtoto wangu Mahmoud na Sham na Adam. Vipi naweza kuipokea habari hii?”
Majeshi ya Ulinzi ya Israel hayakutoa majibu mara moja walipotakiwa kutoa maelezo.
Imekuwa ikipiga mabomu katika eneo la Palestina tangu uvamizi wa Hamas wa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 ambapo maafisa wa Israeli wanasema watu 1,200 waliuwawa.
Siku ya Jumapili (Januari 7), wizara ya afya ya Gaza ilisema shambulizi la Israel limeuwa Wapalestina 22,835 hadi sasa.
“Ulimwengu lazima uone kwa macho yao na siyo kwa macho ya Israel. Ni lazima isikilize na kuangalia kila kinachotokea kwa Wapalestina. Nini alichofanya Hamza kwao na nini ambacho familia yangu imewafanyia? Nini walichofanyiwa na raia wa Ukanda wa Gaza? Hawa wote hawajafanya kitu chochote," alisema Al-Dahdouh.
Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari, chombo cha kimataifa kinachofuatilia waandishi, kilisema Jumamosi, waandishi 77 na wafanyakazi wa vyombo vya habari waliuwawa, kati yao Wapalestina 70, Waisraeli wanne na Walebanon watatu. - Reuters
#Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh
#Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu #jerusalem #alaqsa #msikiti #ibada #ijumaa #gaza #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera