Mwandishi wa Al Jazeera Wael Al-Dahdouh akisalia jeneza la mwanafamilia mwengine

  • | VOA Swahili
    327 views
    Mtoto wake, Hamza Al-Dahdouh, aliuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli akiwa kwenye gari karibu na Rafah pamoja na Mustafa Thuraya, kulingana na maafisa wa afya na umoja wa waandishi wa habari huko Gaza. Wapalestina wote wawili walikuwa waandishi wa habari wa kujitegemea. Wa tatu alikuwa mwandishi wa kujitegemea ambaye alijeruhiwa. Al- Dahdouh alikuwa akifanya kazi na Al Jazeera, ambako baba yake ni mwandishi kiongozi huko Gaza. Wael Al-Dahdouh alikuja kuwa mashuhuri kwa watazamaji kote Mashariki ya Kati baada ya kufahamu wakati wa matangazo mubashara kuwa mke wake, mtoto wake mwengine wa kiume, binti yake na mjukuu wake wa kiume walikuwa wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli. Majeshi ya Ulinzi ya Israel hayakutoa majibu mara moja walipotakiwa kutoa maelezo. Imekuwa ikipiga mabomu katika eneo la Palestina tangu uvamizi wa Hamas wa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 ambapo maafisa wa Israeli wanasema watu 1,200 waliuwawa. Siku ya Jumapili (Januari 7), wizara ya afya ya Gaza ilisema shambulizi la Israel limeuwa Wapalestina 22,835 hadi sasa. Mzozo huu umekuwa ni maangamizi kwa waandishi. Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari, chombo cha kimataifa kinachofuatilia waandishi, kilisema Jumamosi, waandishi 77 na wafanyakazi wa vyombo vya habari waliuwawa, kati yao Wapalestina 70, Waisraeli wanne na Walebanon watatu. -Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu #jerusalem #alaqsa #msikiti #ibada #ijumaa #gaza #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera