- 318 viewsAliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), Wafula Wanyonyi Chebukati, aliaga dunia jana Alhamisi katika hospitali moja mjini Nairobi akiwa na umri wa miaka 63, baada ya kuugua kwa muda mrefu, kama ilivyothibitishwa na familia yake. Chebukati aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa IEBC mwaka 2017 na Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta. Kipindi chake kama mwenyekiti wa tume hiyo kilikumbwa na changamoto nyingi zikiwemo za kusimamia chaguzi za mwaka 2017 na 2022 zilizoghubikwa na utata. Matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2017 yalibatilishwa na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kasoro, na kusababisha uchaguzi wa marudio. Katika uchaguzi wa 2022, Chebukati alimtangaza William Ruto kama Rais mteule, akimshinda mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga, huku kukiwa na mgawanyiko ndani ya tume hiyo. Makamishna wanne walipinga matokeo hayo na kusababisha mtafaruku mkubwa wa kisisa katika taifa hilio la Afrika Mashariki. Licha ya mzozo wa ndani na shinikizo kutoka nje, Chebukati aliendelea kutetea matokeo yaliyotangazwa, ambayo baadaye yaliidhinishwa na Mahakama ya Juu. Kipindi chake pia kilikumbwa na matukio ya kusikitisha, ikiwa ni pamoja na vifo vya maafisa wa IEBC Chris Msando 2017 na Daniel Musyoka 2022. Rais William Ruto aliomboleza kifo cha Chebukati akimtaja kuwa kiongozi aliyetumikia taifa kwa uadilifu, akisema kuwa kifo chake ni hasara kubwa kwa taifa. Chebukati ameacha mjane Mary Chebukati Wanyonyi, ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Mapato 2023, na watoto kadhaa. - VOA Swahili #IEBC #WafulaWanyonyiChebukati #kifo #maombolezi #Rais #kenya #williamruto
Mwenyekiti wa zamani wa IEBC afariki akiwa na umri wa miaka 63
- 22 Feb 2025 - A 33-year-old woman has died by suicide at Kimicha-Rurii village in Kanyekiine ward, Kirinyaga County.
- 22 Feb 2025 - M23 fighters advanced on several fronts in DR Congo's volatile east Friday as the UN Security Council for the first time called on Rwanda to stop backing the armed group and halt the bloodshed.
- 22 Feb 2025 - Police in Kisumu are pursuing a female suspect accused of stabbing to death a woman believed to be having an affair with her husband in the Nyamasaria area of Kisumu East Sub-County.
- 22 Feb 2025 - Three male students from SEKU University, located in Kwa Vonza, Kitui County died on the spot following a road accident last night.
- 22 Feb 2025 - The accident on the busy highway has left residents horrified.
- 22 Feb 2025 - Several areas in northwest Burundi overwhelmed as more than 40,000 people flee conflict
- 22 Feb 2025 - On Friday, the UK said there would be "consequences" for Rwanda over its alleged role in DR Congo.
- 22 Feb 2025 - In that volatile and charged environment, Chebukati could perhaps be excused for forgetting that, in the eyes of many, he was both a servant of the people and a prisoner of their biases.
- 22 Feb 2025 - Twenty-two-year-old professional cyclist Saldido Leon is set to represent Kenya at the prestigious Spinneys Dubai Challenge that is scheduled for today and tomorrow. Speaking from his home in Kilifi County on Thursday, the Coast Region 2024 Tujiamini…
- 22 Feb 2025 - President William Ruto on Friday, February 21, 2025, had a telephone conversation with US Secretary of State Marco Rubio. In the talks, the two conversed on the ongoing conflict in eastern Democratic Republic of Congo where they reaffirmed their…