Mwili wa mtoto wa miaka minne wapatikana kisimani katika kijiji cha Shikhambi kaunti ya Kakamega

  • | Citizen TV
    1,323 views

    Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha shikhambi kaunti ya kakamega baada ya mwili wa mtoto mwenye umri wa miaka minne kupatikana ndani ya kisima.

    Inasemekana kwamba kijana huyo alikuwa amekwenda kucheza na kisha baadaye mwili wake kupatikana katika kisima cha jirani. Wakaazi wa eneo hilo wamekitaja kisima hicho kuwa hatari huku wakitaka kizibwe ili kuzuia jambo kama hilo kutendeka tena. Mwili huo umepelekwa kwenye hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya kakamega huku uchunguzi ukiendelea.