Mwinjuma aeleza kuna matumaini kwa Tanzania kuingia AFCON 2025

  • | VOA Swahili
    581 views
    Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Hamis Mwinjuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wa kufuzu kuingia kwenye michuano ya Afcon 2025 kati ya Tanzania na DRC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam Tanzania. Baada ya mchezo Naibu Waziri wa Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA alieleza kutoridhishwa na matokeo hayo huku wakionyesha imani juu ya timu hiyo kufuzu fainali za AFCON 2025 zitakazofanyika nchini Morocco. Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wa marejeano wa kufuzu fainali za AFCON 2025 dhidi ya DR Congo kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mabao ya Congo yamefungwa na mshambuliaji Meshack Elia katika dakika za 88 na 90+, nyota huyo akiitumikia Young Boys ya Uswisi katika ngazi ya klabu. Licha ya kupoteza mashabiki wa Stars wamezungumzia mchezo huo wakionyesha ilipokosea. Hadi sasa kwenye msimamo wa kundi H, linaongozwa na DR Congo wenye pointi 12 ambao tayari wamefuzu kwenye fainali hizo, Tanzania (Taifa Stars) nafasi ya pili ikiwa na pointi 4, Guinea nafasi ya tatu pointi 3, Ethiopia ikishika mkia ikiwa na pointi 1. #tanzania #afcon2025 #drc #naibuwaziri #hamismwinjuma #daressalaam #benjaminmkapa #uwanja