Mzozo kati ya shirika la kusambaza umeme nchini KPLC na serikali ya kaunti ya Nairobi

  • | K24 Video
    48 views

    Mzozo kati ya shirika la kusambaza umeme nchini KPLC na serikali ya kaunti ya Nairobi umeibuka mapema leo baada ya askari wa kaunti kumwaga taka nje ya jengo la stima plaza hapa jijini Nairobi kufuatia hatua ya Kenya Power kukata umeme kutokana na deni la serikali ya kaunti ambalo halijalipwa. Suluhu ya vita hivi vya ubabe wa kutoa huduma bora haijapatikana huku pande zote zikizidi kulaumiana