Naibu Gavana wa Meru Isaac Mutuma anachukua nafasi iliyoachwa na Mwangaza na kuapishwa kama Gavana

  • | Citizen TV
    3,934 views

    Wakazi wa kaunti ya meru wamejumuika na viongozi wao kushuhudia kuapishwa kwa Isaack Mutuma M'Enthingia kama gavana katika uwanja wa Mwenda antu. Gavana huyo atakuwa wa nne kuongoza kaunti hiyo ambapo anachukua mamlaka kufuatia kubanduliwa ofisini kw agavana kawira mwangaza. Tukio kama hilo limewahi kushuhudiwa katika kaunti za Nairobi na Kiambu baada ya magavana Mike Sonko na Ferdinand waititu kubanduliwa, na pia katika kaunti ya Bomet kufuatia kifo cha gavana joyce laboso.