'Najua kiu ya Watanzania nikutaka kuona umeme unashuka bei, tuachieni serikali tuchakate...'

  • | VOA Swahili
    1,400 views
    Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Greson Msigwa, amesema kuwa nchi imejipatia chanzo kikubwa cha umeme wa gharama nafuu na kwamba Watanzania wanapaswa kuwa na subira wakati Serikali inachakata na kutekeleza hatua zinazohitajika ili kushusha bei ya umeme. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere, Rufiji, Mkoa wa Pwani. Msigwa alieleza kuwa Serikali imewekeza katika miradi mikubwa ya uzalishaji umeme na kuwa, licha ya kiu ya wananchi ya kuona bei za umeme zikishuka, Serikali haitakimbilia kufanya maamuzi ya haraka bila kutathmini madhara yake. “Tanzania sasa ina umeme wa gharama ya chini zaidi Afrika. Gharama zetu za umeme ni za chini kiasi kwamba tunapata changamoto ya kuvutia wawekezaji wa sekta binafsi. Wawekezaji wanapenda kuwekeza kwenye maeneo ambapo gharama za umeme ni juu ili waweze kupata faida kubwa,” alisema Msigwa. Aidha, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata umeme kwa bei nafuu, huku ikijitahidi kuboresha miundombinu na kuchochea ukuaji wa sekta ya nishati nchini. Ripoti ya Amri Ramadhani, VOA, Tanzania. #gresonmsigwa #msemaji #serikali #rufiji #mkoawapwani #bwawa #mwalimunyerere #gharama #serikali #voa #voaswahili #tanzania