Natembeya Amulikwa: Aagizwa kufika mbele ya Tume ya NCIC.

  • | KBC Video
    74 views

    Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ameagizwa na tume ya maridhiano na mshikamano wa kitaifa NCIC kufika mbele yake kwa madai ya kutoa matamshi yanayoweza kuibua chuki za kikabila. Mwenyekiti wa tume hiyo mhubiri Samuel Kobia, amesema Natembeya anatarajiwa kufika mbele ya tume hiyo tarehe 28 mwezi huu kufafanua kuhusu matamshi ya kudhalilisha yanayodaiwa kulenga jamii moja katika kaunti hiyo ambayo imekuwa ikishinikiza kugawanywa kwa kaunti hiyo. Na anavyotuarifu mwanahabari wetu, Abdiaziz Hashim, tofauti zinaendelea kuibuka kati ya Natembeya na naibu wake Philomena Kapkory ambaye anadai kwamba maisha yake yamo hatarini na akaandikisha ripoti katika asasi husika.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News