- 4 viewsRais wa Kenya William Ruto Ijumaa alimteua waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki kuwa naibu wake mpya, siku moja baada ya baraza la Seneti kupiga kura ya kumtimua naibu wake wa zamani, Rigathi Gachagua. “Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais, kuhusu kuteuliwa kwa Profesa Kithure Kindiki kushika nafasi hiyo ambayo imetokea afisini,” Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula alisema Ijumaa, akiwahutubia wabunge mjini Nairobi. Gachagua, ambaye alikanusha mashtaka yote dhidi yake wakati wa kesi ya kuondolewa madarakani, alimuunga mkono Ruto katika ushindi wake wa 2022 na kusaidia kupatikana kwa kura nyingi kutoka eneo lenye wakazi wengi la kati mwa Kenya. Lakini katika miezi ya hivi karibuni , Gachagua amezungumza kuhusu kutengwa, huku kukiwa na taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari kuwa ametofautiana na Ruto wakati miungano ya kisiasa ikibadilika. Kindiki, mshirika wa karibu wa Ruto, ameshikilia wadhifa wa wizara ya mambo ya ndani katika kipindi chote cha miaka miwili ya Ruto kama rais. Hapo awali aliwahi kuwa seneta wa Kaunti ya Tharaka Nithi na alikuwa mgombeaji mkuu kuwa mgombea mwenza wa Ruto wakati wa uchaguzi wa 2022. Baadaye Bunge litalazimika kupiga kura kuidhinisha uteuzi wa Kindiki kabla ya kuapishwa. #Kenya #seneti #gachagua #kindiki #voa #voaswahili
'Nawaunga mkono wabunge na seneti kwa muelekeo wao...'
- - Duniani Leo ››
- 20 Oct 2024 - I thought our consensual romance was private. Now I'm out of a job - and my coworker isn't.
- 19 Oct 2024 - Detectives from the Directorate of Criminal Investigations (DCI) have arrested two individuals believed to be the masterminds of a spate of robberies targeting female students at Laikipia University main campus.
- 19 Oct 2024 - A US judge on Friday let Google delay opening Android-powered smartphones to rival app shops, suspending a November 1 deadline ordered in an antitrust case brought by Fortnite-maker Epic Games.
- 19 Oct 2024 - Hamas vowed Friday not to release the hostages seized during its October 7 attack on Israel until the Gaza war ends, as it mourned the death of its leader Yahya Sinwar.
- 19 Oct 2024 - Democratic Action Party of Kenya party leader Eugene Wamalwa claims there is a plot to have the courts schedule a hearing at night this weekend to proceed with the impeachment of Deputy President Rigathi Gachagua.
- 19 Oct 2024 - He will be at the helm of the institute for 3 years.
- 19 Oct 2024 - Leaders express optimism about Kindiki's ability to unify the region and transcend traditional political divides.
- 19 Oct 2024 - Kalonzo condemns swift ouster of Gachagua, cites legal flaws
- 19 Oct 2024 - Kindiki on the path to history as Kenya's 13th Number Two
- 19 Oct 2024 - MPs' quick nod, two court orders and fightback on dramatic Friday