Ndoto za wanariadha katika Olimpiki Paris 2024 zitafikiwa?

  • | VOA Swahili
    30 views
    Katika Michezo ya Olimpiki iliyoanza rasmi Ijumaa, zaidi ya wanariadha 10,000 wamekusanyika mjini Paris wakiwa na ndoto ya kushinda medali ya dhahabu, ya fedha au ya shaba. Miongoni mwao ni wanawake kadhaa kutoka nchi za Afrika. Miongoni mwao ni wanawake kadhaa kutoka nchi za Afrika, wengi wao wameshinda changamoto kubwa za kiuchumi na kijamii kufika mjini Paris. Kwa mara ya kwanza katika historia, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), ilisema imefanikisha lengo la usawa wa kijinsia kwenye uwanja wa mashindano katika Olimpiki ya mwaka huu. Olivier anaeleza: “Sasa nikujikita kwenye mashindano sio kuzidiwa na shauku kubwa inayosababishwa na Olimpiki, lakini kufurahia mafanikio madogo kwa kila hatua nitakayopiga. Zimebaki wiki mbili kabla ya kushindana na nina hakika muda wote mashindano yanavyokaribia, wasiwasi utaongezeka. Lakini kwa sasa ni kufurahia kufika Paris.” Kuendesha mitumbwi kwa kasia sio mchezo maarufu barani Afrika. Hata hivyo, timu za mitumbwi kutoka Angola, Misri, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini na Tunisia zitawakalisha bara hilo kwenye michezo ya Olimpiki. Olivier anasema mazoezi ya mchezo huo ni magumu kwa wanawake: “Nimefanya safari hii peke yangu kwa kiasi kikubwa na kwa sababu kuna wanawake wachache wanaoshiriki katika mbio za mitumbwi nchini Afrika Kusini, siku zote imenilazimu kufanya mazoezi kati ya wanaume. Kwa hakika hiyo ni changamoto. Ukosefu wa msaada ni changamoto. Na kuhangaika tu na maisha binafsi na michezo, unajua, kwa sababu huwezi kuzingatia tu kuwa mwanariadha, lazima pia niwe mke.” Licha ya hatua iliyopigwa na wanariadha wanawake, changamoto nyingi zinazokwamisha maendeleo ya wanawake katika michezo bado zipo, ikiwemo kutolipwa mshahara sawa na wanaume, ubaguzi, na mazingira duni ya mazoezi. - Mohammed Yusuf, VOA #olimpiki #michezo #olympicparis2024 #ufaransa #paris #voa #voaswahili #wanawake #jinsia