Ndugu wenye majonzi wakiitambua miili ya wachimba mgodi 20 waliouwawa Pakistan

  • | VOA Swahili
    3 views
    Watu wenye bunduki waliwauwa wachimba migodi 20 na kuwajeruhi wengine 7 huko kusini magharibi mwa Pakistan, afisa wa polisi alisema Ijumaa, huku mamlaka zikilaani tukio hilo, wakati operesheni ya kuwasaka washambuliaji hao ikiendelea. Tukio hili la hivi karibuni katika jimbo la Balochistan lenye ghasia limekuja siku kadhaa kabla ya mkutano mkuu wa usalama ambao mji mkuu huo ndiyo mwenyeji wa mkusanyiko huo. Watu hao wenye silaha walivamia eneo la malazi la machimbo ya mkaa wa mawe huko wilaya ya Duki Alhamisi usiku sana, wakawazingira wanaume hao na kuwapiga risasi, afisa wa polisi Hamayun Khan Nasir alisema. Alisema kuwa washambuliaji hao pia walifyatua roketi na kurusha maguruneti katika mgodi wa mkaa wa mawe na kuharibu vifaa ya kuchimbia mgodi kabla ya kutoweka. - AP #mgodi #machimbo #balochistan #pakistan #polisi #familia #hospitali