Netanyahu akutana na wanajeshi na makamanda

  • | VOA Swahili
    2,411 views
    Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, Jumatatu (Desemba 25) Alikutana na wanajeshi huko Kaskazini mwa Gaza, ofisi yake ilieleza. NetanyaWhu alifuatana na Naibu Mkuu wa Majeshi Meja Jenerali Amir Baram aliongea na wanajeshi na makamanda na kuahidi kuendeleza na mapigano hadi mwisho, iliongeza. “Hatutasitisha vita. Yeyote anayezungumzia kusimamisha mapigano – hakuna kitu kama hicho. Hatutasitisha mapigano. Vita vitaendelea mpaka mwisho,” Netanyahu alisema. Hamas na wanamgambo wadogo washirika wa Islamic Jihad, wote wameapa kuiangamiza Israel, wanaaminika kuwashikilia zaidi ya mateka 100 miongoni mwa wale 240 waliowateka wakati wa shambulizi la Oktoba 7 katika miji ya Israeli, walipowauwa watu 1,200. Tangu wakati huo, Israel imelizingira eneo finyu la Ukanda wa Gaza na kuligeuza kifusi. Takriban watu 20,700 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israeli, ikiwemo 250 katika kipindi cha saa 24 zilizopita, kulingana na taarifa ya mamlaka huko Gaza inayotawaliwa na Hamas iliyotolewa Jumatatu. Maelfu ya watu wanaaminika kuwa wamefariki bado wako chini ya kifusi. - Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mbalimbali #Rafah #Netanyahu #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu