Ni ipi mipango ya kuijenga upya Gaza?

  • | BBC Swahili
    2,072 views
    Viongozi kutoka mataifa ya Kiarabu sasa wanaitaka jamii ya kimataifa kuwasaidia katika mpango wao wa kujenga upya ukanda wa Gaza ulioharibiwa vitani. Viongozi hao wanasema hio ndio njia bora ya kuhakikisha kwamba wakazi milioni mbili wa Gaza wataweza kusalia katika makazi yao.Lakini, Ikulu ya White House pamoja na Israel wamepuuzilia mbali pendekezo hilo, wakisema kwamba linashindwa kuangazia changamoto za wazi zinazoikumba Gaza. Aidha wanasimama na pendekezo la Rais Trump kwamba Marekani idhibiti Gaza na kuwahamisha raia wote wa Kipalestina.