279 views
Duration: 25:28
Muziki wa Afrika Mashariki unaendelea kukua kwa kasi na kuvutia mashabiki ndani na nje ya bara. Katika Makala ya Nyota wa Afrika Mashariki wiki hii tunazungumza na Mutoriah, Provoke na Mulla, wote wakiwa ni maprodusa na wasanii kutoka Kenya na Tanzania ambao wanatupa mtazamo mpya: badala ya mashindano, ushirikiano ndio njia ya kufanikisha muziki wetu. Kauli yao inajiri wakati ambapo kumekuwa mjadala hasa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ni muziki upi bora zaidi kati ya Kenya na Tanzania, au ni muziki upi unaongoza? Mutoriah, Provoke na Mulla wanazungumza na mtangazaji kinara wa BBC Dira ya Dunia TV Roncliffe Odit.
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw