Ongezeko la maambukzi mapya ya HIV laibu wasiwasi

  • | KBC Video
    12 views

    Hatari ya kuambukizwa Virusi vya HIV na ugonjwa wa Ukimwi imeongezeka nchini hasa miongoni mwa wale wanaotumia dawa za kulevya zenye msisimko zaidi kwa kujidunga sindano. Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa yanayotokana na mienendo ya watu na maisha ya kijamii, afisa mkuu Mtendaji, Dk Ruth Laibon-Masha, hali hiyo imekithiri zaidi miongoni mwa wavulana na wanaume katika maeneo ambayo hapo awali hayakuzingatiwa kukabiliwa na tatizo la matumizi ya dawa za kulevya. Anasema kuwa hali hiyo isipodhibitiwa kuna hatari ya kusambaratisha mafanikio ya nchi katika kutokomeza virusi vya HIV na ugonjwa wa UKIMWI.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive