Ouma Oluga ameteuliwa katibu wa afya ya umma huku aangazia changamoto za wahudumu wa afya

  • | Citizen TV
    498 views

    Wakati huo huo, katibu mteule wa afya ya umma Fredrick Ouma Oluga amesema kuwa atafanya mazungumzo na vyama mbalimbali vya wahudumu wa afya ambavyo vinalalamikia misharaha, kupandishwa ngazi, mazingira ya kazi na mengineo ili kutatua mitafaruku ya mara kwa mara. Oluga ambaye amewahi kuongoza mgomo wa madaktari amesema kuwa yuko radhi kutafuta maridhiano ili kuboresha maslahi ya wahudumu wa afya na huduma za afya zikiwemo bima ya sha. Aidha amekiri kuwa ana mali ya thamani ya shilingi milioni 196m.