Papa Francis atuma ujumbe wa sauti kwa mara ya kwanza tangu alazwe

  • | BBC Swahili
    1,465 views
    Papa Francis ametuma ujumbe wa sauti akiwashukuru watu kote ulimwenguni kwa maombi yao baada ya kulazwa hospitalini tarehe 14 Februari. Ni mara ya kwanza kwa Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 kusikika kwa umma tangu aingie hospitali kutibiwa na kugundulika kuwa na nimonia katika mapafu yote mawili. Ujumbe mfupi wa mistari miwili, uliorekodiwa mapema siku hiyo kutoka Hospitali ya Gemelli ya Roma, ulichezwa wakati wa ibada ya usiku ya kumwombea papa katika uwanja wa St Peter's Square huko Vatikani. Mapema wiki hii, Vatican ilitangaza kuwa Papa anaendelea vizuri baada ya kukumbwa na hali ya kushindwa kupumua mara mbili na alikuwa akitumia “mashine ya kupumua,”. #bbcswahili #PapaFrancis #vatcan Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw