Pigo kwa mlimbwende wa gereza la Langata baada ya mahakama kukataa ombi la kupunguza kifungo

  • | KBC Video
    2,804 views

    Aliyekuwa mlimbwende wa gereza la wanawake la Lang'ata almaarufu 'Miss Lang'ata' Ruth Kamande ataendelea kutumikia kifungo chake cha maisha kwa kumuua mpenziwe Farid Mohammed Halim, mnamo mwaka wa 2015. Hii ni baada ya jopo la majaji saba wa mahakama ya Upeo, kutupilia mbali rufaa yake ya kutaka kupunguziwa kifungo au kusikizwa tena kwa kesi dhidi yake. Kamande alitaka kutumia dhana ya mwanamke aliyedhulumiwa na mpenziwe katika utetezi wake, akidai kesi yake inaibua masuala yenye umuhimu kwa umma. Alihukumiwa mnamo mwaka wa 2020 kwa kumuua mpenziwe wakati huo Mohammed Halim kwa kumdunga kwa kisu mara 25.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive