Polisi aliyetoroka kazini kutokana na msongo wa mawazo apewa ushauri nasaha Nairobi

  • | Citizen TV
    5,850 views

    Wiki chache baada ya runinga ya Citizen kuangazia masaibu ya Afisa wa Polisi Clement Erumu aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Elwak Mandera na akatoweka kazini kutokana na msongo wa mawazo baada ya kushuhudia wenzake wote wakiuawa na magaidi, idara ya Polisi imemwagiza aondoke kwao Lorugumu kaunti ya Turkana na aripoti katika makao makuu ya Polisi Nairobi,ili apate ushauri nasaha na kurejeshwa kazini . Na kama anavyoarifu Cheboit Emmanuel, familia ya afisa huyo ambaye alikuwa amezamia kazi ya mjengo kijijini imeishukuru idara ya polisi kwa kuchukua hatua hiyo.