Polisi wanasa bangi ya thamani ya Ksh 8M iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Nyanza hadi Mombasa

  • | Citizen TV
    881 views

    Mkuu wa polisi eneo la Buruburu Francis Kamau anasema kuwa bangi hiyo ilikuwa imepakiwa kwenye magari mawili ikiaminika kusafirishwa kutoka eneo la Nyanza kuelekea Mombasa. Kamau akisema walichukua hatua kufuatia vidokezo kuhusiana na bangi hiyo huku mtu mmoja akizuiliwa na uchunguzi ukiendelea.