Prince Rahim Al-Hussaini ateuliwa kuwa Aga Khan mpya

  • | BBC Swahili
    43 views
    Prince Rahim Al-Hussaini ametangazwa kuwa Aga Khan mpya, kiongozi wa kiroho wa mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ya Ismailia. Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa baba yake Prince Karim Aga Khan, aliyefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 88. Prince Rahim Al-Hussaini Aga Khan V atakuwa Imamu wa 50 wa Waislamu wa Ismailia, ambao wanasema wao ni kizazi cha moja kwa moja cha Mtume Muhammad. #bbcswahili #Agakhan #ismailia Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw