Pwani FM washerehekea siku ya kuzaliwa ya mwanamziki wa Bango Mzee Joseph Ngala

  • | KBC Video
    8 views

    Watangazaji wa kituo cha redio cha Pwani FM walisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanamziki wa Bango Mzee Joseph Ngala kwa mbwembwe na tafrija katika kilabu ya Golden Gate huko Mtwapa, kaunti ya Mombasa.Mzee Ngala ambaye ndiye mwanzilishi wa mziki aina ya Bango alikuwa kiongozi wa bendi ya Bahari Boys katika miaka ya sitini huku akiandaa tamasha na makundi mengine mashuhuri kama vile Hodi boys. Mzee Ngala anawashauri wanamziki wa kizazi hiki kuwa na ukakamavu na nidhamu ya hali ya juu ili kunawiri katika tasnia ya mziki. Baadhi ya nyimbo zake mashuhuri ni Tausi Ndege wangu, Pepeta Bango na Mazoeano miongoni mwa nyingine nyingi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive