Rais aanza ziara ya siku 3 katika eneo la Rift Valley

  • | KBC Video
    126 views

    Wanafunzi katika bonde la Kerio ambalo hukumbwa mara kwa mara na visa vya utovu wa usalama sasa watalipa karo ya shule ya shilingi elfu-5 kwa mwaka kufuatia agizo lililotolewa na rais William Ruto. Rais anayefanya ziara ya siku tatu ya kikazi katika eneo la North Rift alisema kuwa hatua hiyo inanuiwa kuhakikisha kwamba wanafunzi zaidi wanasajiliwa shuleni na kuzikinga familia ambazo riziki zao zilivurugwa kutokana na utovu wa usalama na mafuriko. Rais pia aliagiza wizara ya usalma wa Taifa kuzipa zaidi ya familia elfu moja zilizopoteza makazi kutokana na ujangili makao mapya katika muda wa mwezi mmoja. Mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim anatuarifu zaidi kuhusu ziara hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive