Rais mstaafu Uhuru Kenyatta awarai wananchi kuungana na kutozozana ili taifa lisonge mbele.

  • | K24 Video
    1,057 views

    Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amewarai wananchi kuungana na kutozozana ili taifa lisonge mbele. Akisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa magharibi mwa afrika, uhuru amekuwa akisisitiza umuhimu wa umoja si nchini kenya tu bali barani Afrika. Wakati huo huo, katibu mkuu wa Jubilee, Jeremiah Kioni, amewaambia wakenya, hasa katika eneo la mlima kenya, wasitarajie ushauri au ushiriki wa uhuru katika hali ya kisiasa ya sasa. Haya yanajiri wakati wakenya katika mitandao ya kijamii na hata barabarani wakimtakia rais mstaafu heri ya siku ya kuzaliwa.