Rais Ruto aahidi kuimarika kwa uchumi na huduma mwaka wa 2025

  • | Citizen TV
    1,631 views

    Rais William Ruto ameahidi kuwa mwaka wa 2025 utakuwa wa vitendo na kuwa huduma kwa wakenya zitaimarika. Rais ruto amesema serikali yake itatenga fedha za kutosha kuimarisha sekta ya afya nchini na kuhakikisha kuwa wakulima wamepata mbolea ya bei nafuu kwa wingi. Rais ruto aidha amesema kuwa safari yake ya kuunganisha taifa itaendelea.