Rais Ruto aendelea kutoa michango kwa makanisa licha ya pingamizi kutoka kwa vijana wa Gen Z

  • | Citizen TV
    1,664 views

    Haya yakijiri, Rais William Ruto amesisitiza azma yake ya kuendelea kutoa michango kwa makanisa, huku leo pia akiahidi mchango mwingine kwa kanisa la AIC kaunti ya Uasin Gishu. Akizungumza katika ibada ya shukrani katika kanisa hilo la AIC Fellowship Annex, Rais Ruto aliwakashifu wale wanaopinga michango hiyo wana nia ya kueneza utovu wa maadili nchini.