Rais Ruto ahudhuria fainali za kombe la Gavana Fernandes Barasa, Kakamega

  • | Citizen TV
    3,117 views

    Rais William Ruto ameahidi kwamba Kenya, Tanzania na Uganda zitaandaa Kipute cha CHAN mwezi ujao akisema kwamba serikali itashinikiza mkandarasi kukamilisha uga wa bukhungu. Rais alizungumza katika uga wa Mumias katika fainali za makala ya tatu ya kombe la gavana Barasa ambapo veterans waliwashinda Lirhembe Arsenal kupitia mikwaju ya penalti huku akina dada wa butsotso queens wakiibuka washindi kwa michuano ya wanawake. Washindi walizawadiwa shilingi milioni mbili katika kipute kilichodhaminiwa na shabiki.com miongoni mwa wadhamini wengine.