Rais Ruto asema amezungumza na Marekani kuhusu mzozo wa Sudan

  • | Citizen TV
    5,628 views

    Rais William Ruto sasa ameiingiza Marekani katika mzozo wa Sudan baada ya kumpokea kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili, Mohammad Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, kiongozi wa moja ya pande zinazopigana nchini Sudan. Rais Ruto, kupitia mitandao yake ya kijamii alisema kuwa katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani, Marco Rubio, walijadili jinsi Kenya inavyotoa jukwaa kwa wahusika wa vita vya Sudan. Hata hivyo, maelezo haya hayamo katika taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya kigeni ya Marekani kuhusu mazungumzo hayo..