Rais Ruto atangaza shule kufunguliwa tena Jumatatu wiki ijayo

  • | K24 Video
    62 views

    Rais William Ruto ametangaza shule zitafunguliwa tena Jumatatu wiki ijayo kufuatia ushauri wa idara ya utabiri wa hali ya hewa. Haya yanajiri wakati serikali imesema itawasilisha shilingi bilioni moja zitakazotumiwa kurekebisha shule elfu 1,967 zilizoathirika na mvua kubwa. Hata hivyo bado shule nyingi katika maeneo mbalimbali nchini hazijakarabatiwa huku wazazi na wakuu wa shule wakitilia shaka kama ukarabati utakuwa umefanywa kwa wakati ufaao kufikia hiyo Jumatatu.