Rais Ruto awashutumu viongozi wa upinzani akiwalaumu kwa kukataa kuweka kando maslahi binafsi

  • | K24 Video
    734 views

    Rais William Ruto amewashutumu viongozi wa upinzani akiwalaumu kwa kukataa kuweka kando maslahi binafsi ya kisiasa ili kuijenga kenya iliyo na umoja. Ruto alitoa kauli hii wakati wa ibada ya mazishi ya seneta wa Baringo, William Cheptumo, ambapo viongozi wa kisiasa kutoka vyama mbalimbali walikuwa wamehudhuria. Alisisitiza kuwa hana nia ya kuendeleza migogoro ya kisiasa isiyo na mwisho akiwataka viongozi kuelekeza nguvu zao katika kujenga umoja wa taifa badala ya maslahi ya kibinafsi.