Rais Ruto azuru Meli ya kifahari ya Cruise Liner kutoka Norway Mombasa

  • | KBC Video
    4,834 views

    Rais William Ruto amesema Kenya inatazamia kutoa uidhinishaji wa usafiri wa Kielektroniki wa kuingia kwa wingi kwa watalii wa meli za kifahari katika bandari ya Mombasa. Akihutubia wanahabari katika kituo cha meli ya watalii, rais alisisitiza dhamira ya serikali ya kutangaza nchi hii kama kivutio cha utalii kinachopendelewa. Alizitaka sekta binafsi kutumia fursa ya ongezeko la watalii kuwekeza zaidi katika sekta ya kuwakaribisha wageni. Alisema nchi hii inalenga kukaribisha watalii milioni tano ifikapo mwaka wa 2027, kutoka watalii milioni 2.4 mwaka wa 2024.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive