Rais Trump ajiandaa kuwaenzi kizazi cha watu weusi mabingwa

  • | VOA Swahili
    229 views
    Rais wa Marekani Donald Trump ameungana na taifa katika kumbukumbu ya Mwezi wa Historia ya Watu Weusi kwa kuandaa hafla White House akiwa na mcheza golf maarufu Tiger Woods. Wakati wa hafla hiyo Alhamisi, Trump alitoa hotuba ambapo alipongeza “vizazi vya watu Weusi, mabingwa, wapiganaji na wazalendo, ambao wamekuwa na jukumu kubwa katika kuinyanyua historia ya taifa hili na kutangaza kuweka bustani yenye sanamu za watu weusi kama vile Harriet Tubman, Rosa Parks, Aretha Franklin, Coretta Scott King. “Tutatengeneza baadhi ya kazi nzuri sana za sanaa katika mfano wa sanamu ya wanaume kama Frederick Douglass, Booker T Washington, Jackie Robinson … Martin Luther King Jr., Muhammad Ali … na marehemu Kobe Bryant,” Trump alisema. _ AP #trump #blackhistorymonth #voa