Rais Trump akutana na Fogel baada ya kuachiliwa huru kutoka Russia

  • | VOA Swahili
    72 views
    Rais wa Marekani Donald Trump amemkaribisha Mwalimu raia wa Marekani Marc Fogel katika white house jana jumanne usiku baada ya Fogel kuachiliwa huru kutoka Russia ambako amekuwa akizuiliwa tangu Agosti 2021 kwa tuhuma za kuingia Russia na bangi. Fogel amesema kwamba anahisi ana bahati sana duniani. Ameshukuru rais Trump na wanadiplomasia wa Marekani Pamoja na mawakili kwa kusaidia kuweza kuwa uhuru.  Trump amesema ameshukuru kwamba Russia ilimuachilia huru Fogel. Hata hivyo hajatoa taarifa zaidi kuhusu makubaliano yaliyopelekea Fogel kuachiliwa huru. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba Marekani ilikuwa imekubali kumuachilia huru raia wa Russia anayezuiliwa katika gereza la Marekani kama sehemu ya makubaliano hayo na kwamba aliyeachiliwa huru atatajwa atakapowasili Russia. - VOA NEWS #rais #marekani #marcfogel #whitehouse #russia #bangi #voa #voaswahili