Russia iliionya Marekani kabla ya kufyatua kombora la Oreshnik

  • | VOA Swahili
    4 views
    Msemaji wa Kremlin amesema leo Ijumaa kwamba Moscow iliipelekea Marekani onyo dakika 30 kabla ya kufyatua kombora jipya la masafa ya kati huko Ukraine. Kremlin iliruhusu kufyatuliwa kombora hilo jipya lililopewa jina la Oreshnik dhidi ya mji ulio kati kati mwa Ukraine wa Dnipro jana alhamisi. Rais Putin amesema kwenye hotuba yake kwamba shambulio hilo limefanyika kujibu hatua ya Kyiv wiki hii kutumia makombora ya Marekani na Uingereza yenye uwezo wa kufika mbali ndani ya Russia. Putin alionya kwamba mfumo wa Marekani wa ulinzi wa anga hautaweza kuzuia kombora jipya ambalo anasema lina safiri kwa kasi ya mara 10 zaidi ya sauti. Hii leo pia msemaji Peskov aliulaumu utawala wa hivi sasa wa Marekani kwa kuzorotesha ugomvi wa Ukraine na kusema kwamba hakuna mawasiliano kati ya Moscow na Washington juu ya suala hili. - AP Wakati huo huo Waziri wa ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amesema serikali yake ilikuwa inaongeza uwezo wa ulinzi wa anga wakati ikijibu mashambulizi ya makombora ya masafa marefu ya Russia katika mji wa ukarine wa Dnipro. Umerov ameyasema hayo leo katika maelezo yake kwa vyombo vya habari akiwa na mwenzake wa Sweden Pal Johnson mjini Stockholm. Jonson ameongeza kuwa shambulizi la Russia haliwezi kuikatisha tamaa uungaji mkono wa serikali yake kwa Ukraine. Alhamisi Russia ilifyatua makombora ya masafa marefu kujibu hatua ya Marekani na Uingereza kuiruhusu Kyiv kushambulia ndani ya ardhi ya Russia na silaha zake za Magharibi za ubora wa juu. - AP and Reuters #voaswahili #afrika #ukraine #russia #kombora #oreshnik #dnipro #moscow #russia