Ruto ashauriana na vijana wa Gen-Z mtandaoni

  • | KBC Video
    1,206 views

    Rais William Ruto ameahidi kwamba maafisa wa polisi walionaswa kwa kamera wakipiga risasi ovyo kwenye umati wa watu wakati wa maandamano ya kupinga muswada wa fedha wa mwaka 2024 wakachukuliwa hatua za kisheria. Akizungumza wakati wa mdahalo na vijana kupitia kitandazi cha X, Ruto alionya kuhusu usambazaji wa taarifa ghushi kumhusu mvulana wa umri wa miaka 12 aliyefariki baada ya kudaiwa kupigwa risasi mara nane mtaani Ongata Rongai. Ripota wetu Abdiaziz Hashim ana mengi kuhusiana na mdahalo huu baina ya Rais na vijana ambapo walijadiliana masuala kadhaa miongoni mwayo dhulma za polisi, kukamatwa kinyume cha sheria, mabadiliko katika serikali na katiba ya tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC)

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive