- 4,536 viewsDuration: 2:14Rais William Ruto ametia saini sheria ya kudhibiti mashirika ya serikali itakayounda hazina ya kitaifa ya miundo msingi. Sheria hiyo pia itasaidia kusaka shilingi trilioni 5 za kufadhili mikakati yake ya kupandisha taifa hadi kiwango cha mataifa yaliyostawi zaidi duniani. Akizungumza katika hafla ya kuhitimu kwa wanafunzi wa chuo cha ulinzi huko Nakuru, rais alisema kenya imechelewa sana katika safari ya kufikia viwango vya mataifa kama vile Singapore, Malaysia na Japan