Ruto: Kuna ufanisi katika nusu ya kwanza ya hatamu yake

  • | KBC Video
    93 views

    Rais William Ruto amesema Kenya imepiga hatua muhimu za maendeleo katika kipindi cha nusu ya kwanza ya utawala wa Kenya Kwanza. Rais Ruto alisema kwamba serikali imefanikiwa kuanzisha miradi yake, ikanakili ukuaji katika sekta ya kilimo na kuimarisha uchumi, akiahidi mageuzi zaidi katika siku za usoni. Akizungumza alipoungana na waumini wa kanisa la AIC Fellowship Annex, Eldoret, Uasin Gishu kwa ajili ya ibada ya Jumapili, Rais Ruto aliwahakikishia wakenya kwamba taifa hili liko kwenye mwelekeo unaofaa. Rais Ruto pia alielezea ufanisi wa maeneo ya kiuchumi, akikariri kwamba ukuaji wa uchumi umewezesha kutengwa kwa raslimali zaidi kwa ajili ya ujenzi wa miundomsingi. Aidha Rais Ruto alisisitiza kwamba maendeleo na umoja vinaambatana, kwani taifa lenye umoja huafikia ufanisi kwa urahisi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive