Rwanda inaadhimisha miaka 30 tangu mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi

  • | West TV
    9 views
    Tarehe 7 aprili inaadhimisha miaka 30 ya mauaji ya halaiki ambayo yalishuhudia karibu watutsi milioni 1 na Wahutu wenye msimamo wa mkali wakiuawa nchini rwanda. makovu kwenye miili ya walionusurika yanawakumbusha wanyarwanda kuhusu mauaji hayo. zaidi ya watu milioni 1 - wengi wao kutoka kabila la Watutsi walio wachache, lakini pia wahutu walio wengi waliojaribu kuwalinda Watutsi - waliuawa kwa utaratibu na wahutu wenye msimamo mkali wakati wa mauaji ya siku 100 yaliyoanza aprili 7, 1994. Umoja wa mataifa unafanya matukio ya kuwakumbuka wahasiriwa na kuwaenzi walionusurika. Wahutu wenye itikadi kali walikuwa wakiwawinda vijana ambao waliwashuku kuwa wanashirikiana na rwandan patriotic front (RFP), kundi la waasi wengi wa kitutsi waliongozwaa na Paul Kagame, ambaye ambaye baadaye alichua wadhifa wa urais Matukio hayo ya kusikitisha yalichochewa na mauaji ya rais wa kihutu juvenal habyarimana usiku wa tarehe 6 aprili 1994. ndege yake ilitunguliwa Kigali na Wahutu wenye msimamo mkali na wanamgambo wa interahamwe. Mauaji hayo yalianza siku iliyofuata na kudumu kwa siku 100, na kugharimu maisha ya watu 800,000. ingawa wengi walikuwa watutsi, wahutu wenye msimamo wa wastani pia waliuawa. Wengine waliuawa na majirani zao katika wimbi la ghasia za ajabu. Wahasiriwa wao walipigwa risasi, kupigwa au kukatwakatwa hadi kufa katika mauaji yaliyochochewa na propaganda za kupinga Watutsi zilizotangazwa kwenye runinga na redio.nchini humo kulingana na takwimu za umoja wa mataifa takriban wanawake 100,000 hadi 250,000 walibakwa, Mamia ya maelfu ya watu, hasa wa kabila la wahutu wakihofia mashambulizi ya kulipiza kisasi, walikimbilia nchi jirani ikiwa ni pamoja na jamhuri ya kidemokrasia ya kongo,. kwingineko Maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya israel wamekusanyika mjini tel aviv, miongoni mwa maeneo mengine ya nchi, kuitaka serikali kufikia makubaliano ya kuwaachilia huru idadi kubwa ya mateka wanaoshikiliwa na kundi la hamas huko gaza na kufanya uchaguzi wa mapema. waandamanaji hao katika maandamnao yao walioonyesha kugadhabishwa na serikali ya Benjamin Netanyahu kwa kushindwa kwake kuwaachilia mateka hao baada ya miezi sita ya mapigano. vyombo vya habari vya israel viliripoti matukio ya makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji huko Tel Aviv, ambapo waandamanaji waliripotiwa kuwasha moto mara kadhaa, kabla ya kuzimwa haraka na polisi. watu waliimba "polisi, polisi mnamlinda nani hasa?", na "ben-gvir ni gaidi", wakirejelea waziri wa usalama wa taifa wa israel, gazeti la haaretz liliripoti. waandalizi wa maandamano walionukuliwa na vyombo vya habari vya ndani walisema mikutano ya hadhara ilikuwa ikifanyika katika maeneo mengine takriban 50 nchini kote pamoja na tel aviv. maandamano ya hivi punde yanakuja wakati mazungumzo ya kusitisha mapigano - ambayo yanajumuisha majadiliano kuhusu kuachiliwa kwa mateka - yanapangwa kufanyika cairo. mazungumzo hayo yanasimamiwa na qatar, misri na marekan