SADC na EAC wakutana kuhusu DRC

  • | BBC Swahili
    8,500 views
    Mawaziri kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, na ile ya kusini mwa Afrika, SADC, wamewasili mjini Dar es Salaam, Tanzania kuanza mkutano wa siku mbili kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro nchini DRC. Mkutano huo unajiri wakati Marekani ikionya kuhusu uwezekano wa kuweka vikwazo dhidi ya maafisa wa Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuhusiana na hali ya usalama mashariki mwa DRC.