Seneta Mandago ashtakiwa kwa kesi ya sakata ya elimu Uasin Gishu

  • | Citizen TV
    2,236 views

    Kesi ya ubadhirifu wa fedha za hazina ya elimu kaunti ya Uasin Gishu inayomkabili seneta wa kaunti hiyo Jackson Mandago imeanza kusikizwa hii leo, katika mahakama ya nakuru. Shahidi wa kwanza Joel Chelule amekana kwamba ndiye mwenyekiti wa hazina hio ya shilingi bilioni moja na badala yake kufichua kwamba alijulishwa kuwa ni mmoja wa wadhamini baadaye.