Serikali hatimaye yaondoa mapendekezo tata ya ushuru

  • | KBC Video
    17 views

    Kamati ya bunge la kitaifa imependekeza kuondolewa kwa ushuru uliopendekezwa wa mkate, mafuta ya kupikia, magari, ubadilishanaji fedha na ushuru wa kuzuia uchafuzi wa mazingira. Hii inafuatia shinikizo za wananchi waliolalamikia baadhi ya vipengee vya mswada wa fedha wa mwaka 2024. Kwenye kikao na wanahabari, kamati hiyo ilisema imetilia maanani maoni ya umma na hivyo kufanyia marekebisho mswada huo kwa lengo la kuwapunguzia Wakenya mzigo wa ushuru. Tangazo hilo lilifuatia mkutano wa wabunge wa mrengo wa Kenya Kwanza katika Ikulu ya rais jijini Nairobi uliohudhuriwa na rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua. Ripota wetu Abdiaziz Hashim anatufafanulia kuhusu athari za mapendekezo ya kamati hiyo huku wataalamu wa masuala ya kiuchumi wakitahadharisha kwamba hazina kuu inakumbwa na kibarua kigumu cha kuziba nakisi ya bajeti endapo bunge litaidhinisha marekebisho hayo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive