Mwanahabari mashuhuri kaunti ya Busia afariki kutokana na ugonjwa wa saratani

  • | Citizen TV
    228 views

    Serikali imehimizwa kuweka vifaa vya kisasa vya kupima na kutambua ugonjwa wa saratani katika hospitali za umma ili kuwezesha madaktari kutambua ugonjwa huo kabla ya kuenea sana. Ndio wito uliotolewa na familia ya mwanahabari mkongwe zaidi katika kaunti ya busia john ojanji ambaye alifariki akipokea matibabu ya saratani ya tezi dume katika hospitali moja kaunti ya siaya.marehemu alikuwa mtangazaji wa runinga ya western nyota na radio ya bulala fm na alipatikana na ugonjwa huo mwaka mmoja uliopita .familia yake imesema kuwa serikali za kaunti zimeonekana kulemewa na utoaji wa huduma stahiki za matibabu ya kitaalamu, hali inayochangia maafa zaidi.