Serikali itakopa jumla ya bilioni mia nane sitini na moja

  • | K24 Video
    31 views

    Serikali sasa itakopa jumla ya bilioni mia nane sitini na moja huku ikihofiwa kuwa kiwango hicho kitafika shilingi trilioni moja katika mwaka huu wa kifedha kufuatia nia ya serikali ya kulipa madeni ya wakandarasi, pia hofu hiyo inatokana na ushuru uliolengwa kupunguzwa kwa shilingi bilioni tisini na tatu. KRA katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa kifedha imekosa kuafikia malengo yake kwa shilingi bilioni thelathini na saba, ambayo vilevile imepelekea kupunguzwa kwa makadirio ya bajeti ya mwaka ujao wa kifedha.