Serikali yaafikia pendekezo la kufunga maziara ya Lang'ata

  • | Citizen TV
    3,676 views

    Huenda makaburi ya Lang’ata yasitumike tena kuzika Wakenya baada ya wizara ya afya kukubaliana na mapendekezo ya jopo lililobuniwa kuchunguza hali katika eneo hilo la makaburi. Hatua hii inatokea miaka 20 baada kutangazwa kuwa makaburi ya Lang’ata yamejaa na hayastahili kutumika kwa shughuli za kuzika. Sasa kizungumkuti ni kutimizwa kwa pendekezo la kuchukua tena ardhi iliyoko karibu na makaburi hayo na ambayo ilinyakuliwa na kujengwa nyumba za makaazi.