Serikali yakosolewa kwa kufanya mzaha na utekaji nyara

  • | Citizen TV
    835 views

    Viongozi wa makanisa sasa wamewakashifu baadhi ya viongozi serikalini kwa kufanya mzaha na maswala ya utekaji nyara humu nchini. Wakati wa ibada maalum ya familia zilizoathirika katika eneo la Maseno kaunti ya Kisumu viongozi walizitaka asasi za serikali kuchukua hatua na kuhakikisha usalama wa wakenya wote. Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti pia aliwafokea baadhi ya viongozi kwa kueneza hulka mbaya mtandaoni, Kama Laura Otieno anavyoarifu