Serikali yasema madarasa yatakuwa tayari mwakani

  • | KBC Video
    4 views

    Katibu katika idara ya elimu ya msingi, Belio Kipsang, amewahakikishia Wakenya kuwa serikali inajitahidi kutekeleza ipasavyo mtaala mpya wa masomo ya umilisi almaarufu CBC. Akizungumza katika afisi ya kamishna wa kaunti ya Meru, aliposimamia ufunguzi wa kontena ya mtihani wa kidato Cha nne; Kipsang alisema wizara ya elimu tayari imejenga madarasa 3,500 yatakayotumiwa na wanafunzi wa gredi ya 9 katika awamu ya kwanza huku madarasa mengine 7,500 yakiendelea kujengwa kwa awamu ya pili. Kipsang aliongeza kuwa ifikapo tarehe 15 mwezi Disemba, madarasa yote yatakuwa yamekamilika.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive