Serikali yatakiwa kuwawajibisha wauaji wa Lucy Wamaitha

  • | KBC Video
    70 views

    Viongozi wa kisiasa, kidini na wananchi, wametoa wito kwa vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi na kuwafungulia mashtaka washukiwa wa mauaji ya Lucy Wamaitha. Lucy Wamaitha mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa akifanya kazi katika shirika moja lisilo la serikali katika kaunti ya Kiambu, alitoweka mnamo Januari 16 mwaka huu akiwa kwenye ziara ya kikazi akiambatana na mkubwa wake kazini. Inadaiwa alitoa taarifa kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika shirika hilo. Sehemu za mwili wake zilipatikana baadaye kwenye mfuko zikiwa zimetupwa katika mto Sagana.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive