Katibu Mkuu katika wizara ya Elimu, Julius Bitok amewahakikishia watahiniwa wa mtihani wa sekondari msingi (KAPSEA) na wale wa Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi (KJEA) kwamba wataweza kufanya mitihani yao bila tashwishi licha ya changamoto zinazoweza kutokea. Bitok amesema mitihani inaendelea vizuri na wadau wote wako makini kushughulikia changamoto ibuka kuhakikisha shughuli hiyo inaendelea kwa uadilifu, uhuru na haki. Amekariri kuwa wizara ya elimu inashirikiana na vitengo vya usalama ili kuzuia udanganyifu wowote wa mtihani.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive